Home  |  Shelly  |  The Calmes  |  Neema House Church  |  Manna  Care Center 
Help Us  |    Contact Links  |  TUFUNDISHE Kigazeti


TUFUNDISHE Kigazeti

Pata Mawazo ya Chapchap Kuinua Kipindi Chako

 

YESU NI BWANA WANGU, NA HUU NI USHUHUDA WANGU!

Watie moyo watoto na vijana na uwapatie nafasi ya kutoa ushuhuda kuwa wao ni “Mali ya Bwana”. Anza kwa wewe mwenyewe kuwatolea ushuhuda wako, ili wanafunzi kwa kutumia ushuhuda wako wajifunze. (Uwe na maneno rahisi na mafupi sio magumu na marefu.) Kisha baada ya wewe kutoa ushuhuda wako wa wokovu wako, muulize mwanafunzi yeyote ajitolee kutoa ushuhuda wake jinsi alivyompokea Yesu.

Jaribu kuwatengenezea maneno rahisi ya kuwaongoza na uyabandike katika ubao wowote hapo darasani ili wakumbuke mara kwa mara vitu muhimu katika ushuhuda. Wanafunzi wanaweza kusoma na kujaza hayo mapengo na baadaye wataweza kumshuhudia Yesu vizuri kabisa mbele ya wengine.

Nilijua kuwa ninahitaji Mwokozi kwa sababu______________________________________________________.”

Nilipomwomba Yesu aniokoe nilikuwa na umri wa miaka_____.”

"Kuanzia siku hiyo Mungu amekuwa msaada wangu katika________________________________________.”

Nampenda Yesu, kwa sababu ____________________.”
 

TUFUNDISHE April/May 2008 Vol. 1 No. 6

Back to index

 
Animated flag by
 
www.3DFlags.com
Web Editor - Don Tarvin
Updated 26 Sep 2008