 |
TUFUNDISHE Kigazeti
Njia ya Kufundisha Maombi |
MUNGU ANATAKA KUTUSIKILIZA SISI
LENGO: Kuwasaidia wanafunzi watambua umuhimu wa mawasiliano kati
yetu sisi na Mungu Baba yetu.
Wasaidie wanafunzi wajue kuwa Mungu anataka sisi tuongee naye muda
wowote na mahali popote, iwe nyumbani, katika gari, kanisani, shule,
sokoni, nje au kiwanjani. Haijalishi muda gaani na sehemu gani.
Endelea kuwaelezea wanafunzi kuwa ingawa Mungu hatumwoni kwa macho
yeye bado yupo pamoja nasi na anataka sisi tuongee naye popote
tunapokuwa. Nafikiri tusijisikie vibaya au kujihisi wapweke kama uko
na mtu halafu yeye anakuwa hakujali anakuwa kama ana shughuli zake
tu.
Toa mfano huu: Wanafunzi wawili wawili watoke mbele kundi mojamoja.
Kisha katika hilo kundi la wanafunzi wawili mmoja azungumze na
mwenzie. Na huyo mwenzie awe hata hamsikilizi wala kumjali huyu
anayeongea naye. Aangalie pembeni tu na kufanya shughuli zake. Kisha
muulize yule aliyekuwa akiongea anajisikiaje? Pengine atasema
alijisikia kukataliwa na hata hasira kidogo pengine.
Waambie wanafunzi kuwa vivyo hivyo Mungu naye hujisikia kukataliwa
na kusahauliwa pale tunapokuwa hatuongei naye au kutambua uwepo
wake. Anaweza hata asijisikie hasira bali atajisikia kukosa
ushirikiano na sisi.
Wakumbushe kuwa Mungu daima hatuachi sisi wapweke. Yupo nasi muda
wote. Kila siku Yeye yupo tayari kusikiliza matatizo yetu, mahitaji
yetu na shukurani zetu. Anataka kushirikiana na sisi katika kila
kitu tunachokifanya na kutusaidia kwa njia yoyote awezayo. Na
tunaweza kuongea na Mungu kwa njia ya maombi tu.
TUFUNDISHE April/May 2008 Vol. 1 No. 6
Back to index
|