 |
TUFUNDISHE Kigazeti
Neno la Mungu Kuhusu
Uinjilisti Wa Watoto |
KUWASADIA WATOTO KUKUA KIROHO
Itakuwa ni ajabu na kitu cha kushangaza sana iwapo mtoto ataweza
kutambua mahitaji yake ya chakula cha kiroho kama anavyohitaji
chakula cha kawaida kama nyama. Watoto wanahitaji kujua jinsi ya
kutii amri iliyopo katika 2 Petro 3:18, “Lakini kueni katika neema
na katika kumjua Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo”. Pia watoto
wanahitaji kutiwa moyo na kutambua maendeleo yao ya kiroho.
Wafundishe watoto katika njia hizi nne na uwe tayari kuwasaidia.
1. KWENDA KANISANI KWENYE DARASA LA WATOTO
Wahimize watoto wampe Mungu muda waeleze umuhimu alioutoa Mungu
katika kukusanyika pamoja kumwabudu. Waebrania 10:25, “Wala tusiache
kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane;
na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa
inakaribia.”
Wafundishe kuwa makini katika kusikiliza Neno. Watie moyo kuuliza na
kujibu maswali ya udadisi kama: Nani? Nini? Lini? Wapi? Kwa nini?
Mfano wa Maswali:
* “Somo la leo linafundisha kuhusu nani?”
* “Nini kilitokea katika somo la leo?”
* “Je, ilitokea lini?”
* “Je, somo hili inapatikana wapi kwenye Biblia?”
* “Je, ni kwa nini somo hili ni muhimu kwangu?”
Kama ukiuliza mara kwa mara maswali haya, basi utakuwa umejenga
maswali haya akilini mwao. Mwishowe wataanza kujiuliza maswali haya
wenyewe na kujikuta wameanza kujilisha chakula cha kiroho wenyewe
kanisani.
2. KUSOMA NENO LA MUNGU NA KUOMBA
Wasaidie watoto waweke kipindi cha peke yako na Mungu kwenye ratiba
zao za kila siku. Ingawa watoto wa siku hizi wanajali sana na
kutambua umuhimu wa muda kwa kupitia kutiwa moyo na kuhimizwa
wanaweza kutenga hata dakika 10 au 15 kusoma Neno, kujikumbusha
mistari ya Biblia na kuomba.
|
Je, wanapaswa kusoma nini?
Tumia kitabu cha masomo ya watoto pamoja na Biblia ya watoto.
Anzisha usomaji wa Biblia ya watoto nzima katika njia rahisi
na inayoweza kueleweka wasome mistari michache kwa kila siku.
Ili waweze kujilisha Neno la Mungu wanaposoma wanapaswa
kujiuliza maswali haya. |
|
“Je, mstari huu au maneno haya yanasemaje?”
“Je, maana yake ni nini?”
“Je, Mungu ananiambia nini hapa?” |
Kama watapata nafasi ya kuandika majibu kwenye daftari itakuwa ni
rahisi kuwa kujifunza kwa undani kuhusu mistari hiyo ambayo Mungu
anasema.
Soma Timotheo 4:13
Je, wanapaswa kujikumbusha nini?
Ni vizuri kama watajikumbusha mstari waliopewa na mwalimu kujifunza
na mstari ambao umewagusa na kuongea na mioyo yao; pia mistari
ambayo inafahamika na wengi kama vile Zaburi 1 au Zaburi 23.
Je, mtoto ale kwa muda gani kila siku? Kama jinsi chakula cha mwili
kinavyowatia nguvu watoto, ndivyo jinsi ulaji wa mara kwa mara wa
Chakula cha Kiroho unavyowajenga na kuwatia nguvu kiroho.
3. KUMTII MUNGU SIKU KWA SIKU
Soma kwa makini 1 Yohana 2:3. Na katika hili twajua ya kuwa tunamjua
yeye ikiwa tunazishika amri zake. Pia mtoto hupata Chakula cha
Kiroho hata anaposikiliza sauti ya Mungu.
Mchezaji mmoja alipokuwa katika dakika za mwisho za mchezo timu
yake ilifungwa goli lingine la ushindi lakini, badala ya kukasirika
na kuchukia, alimwambia Mungu amtie nguvu ili awe mchezaji mwema.
Huyu alimtii Mungu na kumtegemea.
Mtoto wa Mungu lazima awe tofauti popote anapotembea. Hebu waulize
watoto swali hili, “Je, Mungu alikusudia vipi ili umtii yeye
katika wiki iliyopita?” Wachukue nafasi ya kumsifu Mungu kwa
jinsi alivyofanya kazi kwa watoto ili wafanye mapenzi yake. Soma
Wafilipi 2:13.
4. KUTOA USHUHUDA
Mtoto hupenda kuwashirikisha wenzie juu ya imani yake. Mtu anayetoa
ushuhuda ni yule anayetoa ushahidi. Hivyo basi, watie moyo watoto
kutoa ushuhuda siyo tu juu ya wokovu, bali pia jinsi Mungu
anavyofanya kazi ndani yao.
Mtoto anaweza kuwaeleza wenzake jinsi Mungu alivyojibu maombi yake,
jinsi alivyojifunza kutoka kwenye Neno la Mungu, jinsi Mungu
alivyompa ujasiri wa kuwapongeza wachezaji wa timu nyingine ingawa
timu yake ilishindwa, na jinsi Mungu alivyomsaidia asiende kuangalia
video mbaya.
Kama mtoto mmoja ataweza kutoa ushuhuda na jinsi Mungu alivyofanya
kazi ndani yake, watoto wengine watatiwa moyo kusimama imara pia.
Ikiwa watajengewa msingi wa nidhamu hii ya maisha ya kikristo, basi
wataendelea kukua hata wakiwa peke yao.
Ni wajibu wetu kuwafundisha watoto jinsi vile Mungu
anavyofanya kazi kwenye maisha ya watu wengine, ili waweze kujifunza
na kuona kweli Mungu anaweza kubadilisha maisha ya watu na
inawezekana kabisa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Pia, tuwatie
moyo katika maisha yao ya kiroho kila siku ili waweze kusonga mbele
katika maisha yao ya kila siku.
TUFUNDISHE April/May 2008 Vol. 1 No. 6
Back to index
|