 |
TUFUNDISHE Kigazeti
Maswali Magumu Yaulizwayo na Watu
WENGI |
Je, Mungu bado anaendelea kufufua wafu hadi siku hizi?
Katika kipindi cha Biblia Mungu
mara nyingine alifufua watu waliokufa wakawa na afya tena. Na
alitumia watu wake maalumu kufanya muujiza huu wa aina yake. Soma
Wafalme 17:24, Luka 7:16, Yohana 11:42-45 na Matendo 9:40-42.
Aliwatumia manabii (Elisha na Elia). Alitumia mtoto wake (Yesu)
pekee. Aliwatumia mitume (Petro na Paulo) pia. Watu hawa
walihakikisha katika namna ya kushangaza sana kuwa maneno yao
yalitoka kwa Mungu. Hivyo maneno hayo (na maneno ya wengine Mungu
aliowachagua) yaliandikwa kisha baadae yakaunganishwa na kuitwa ‘Biblia’.
Mungu bado ana uwezo wa kuwafufua watu kutoka katika wafu na tayari
ameshatuonyesha sisi uwezo wake huo katika Biblia. Hivyo tunaweza
kuamini tu kwamba uwezo huo anao. Sio lazima hadi tuone mtu
amemfufua mtu aliyekufa. Hili ndiyo tuamini kuwa Mungu anaweza. Watu
wakikataa kuliamini Neno la Mungu hata wakimuona mtu anafufuka toka
kwa wafu haitoshi kuwashawishi kuwa ni kweli. Soma Luka 16:31.
Mungu ataendelea kuwa na uwezo huo wa kufufua wafu hata kama
alifanya siku hizo au hata asipofanya. Yesu atakaporudi mara ya pili
atamfufua kila Mkristo. Ila hautakuwa na mwili wako huu uliouzoea
kama wa Lazaro aliyefufuliwa na Yesu au wa wale wengine
waliofufuliwa. Tunasoma habari zao katika Biblia.
Utapata mwili mpya kama ule Yesu aliokuwa nao ule ambao hautakufa
tena bali utaishi milele. Soma 1 Wakorintho 15:35-58 na 1
Wathesalonike 4:26.
Back to index
TUFUNDISHE April/May
2008 Vol. 1 No. 6
|